Tenzi Za Rohoni
Tenzi za Rohoni ni programu inayojumuisha mkusanyiko wa nyimbo 161 kutoka katika kitabu cha Tenzi Za Rohoni kwa lugha ya Kiswahili. Programu hii imeandaliwa kukuwezesha kumwamudu Mungu kwa njia ya uimbaji mahali popote na muda wowote. Sifa za program ni kama zifuatazo:- • Inahusisha eneo la utafutaji ambapo unaweza kutafuta wimbo kwa namba au kwa neno unalokumbuka liwe jina la wimbo kwa Kiswahili, kwa kiingereza au maneno yaliyo ndani ya wimbo. • Inakuwezesha kuweka nyimbo unazozipenda katika orodha tofauti na hivyo kuupata kwa urahisi wakati mwingine, pia unaweza kuuondoa pale unapoona inafaa. • Inakuwezesha kufuatilia wimbo kwa njia ya ala za sauti (thanks to hymnserve.com for the accompaniments). • Inakuwezesha kucheza ala hata ukiwa haupo kwenye programu • Inakuwezesha kuona wimbo unaocheza ala ukiwa kwenye nyimbo zingine. • Inakuwezesha kuona wimbo uliofungua mara ya mwisho kwa kuuangaza. • Inakuwezesha kukuza ukubwa wa maandishi wa maneno ya wimbo kadri unavyoona inafaa. • Inakuwezesha kushiriki maneno ya wimbo na ndugu jamaa na marafiki kwa urahisi. • Inakuwezesha kubadili muonekano wa programu unaofaa katika mazingira ya Mwanga au Giza ili kuwezesha uono usioumiza macho.